Ukifuatilia vizuri taarifa za kituo cha utafiti na ushauri cha Gartner, unasema kuwa simu milioni 344.3 zinazotumia Android ziliuzwa katika robo ya pili ya mwaka 2016.
Mauzo hayo ya Android kwa upande mwingine ni ongezeka la asilimia 4.3 (namba hii inaweza ikaonekana ni ndigo ila katika biashara ina maana kubwa sana).
Hapa inamaana simu za Android kwa vipindi vya nyuma hazikununuliwa kwa wingi kama kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2016.

Katika Robo hiyo inaonyesha dhahiri kuwa Samsung ndio kaongoza kuuza simu duniani kote katika robo hiyo ya pili ya mwaka 2016. Samsung imeuza si chini ya simu milioni 76.7.
Kwa upande wa Apple yenyewe imeuza simu milioni 44.3 namba hii ni ndogo hivyo inaifanya Samsung kuwa kidedea katika mauzo.
Huawei ikifuatia ikiwa na mauzo ya simu milioni 30.6, OPPO milioni 18.4 na Xiaomi milioni 15.5
SOMA PIA:Â Apple Na Samsung Watupwa Mbali: Huawei Imeongoza Mauzo China Katika Robo Ya Pili Ya 2016!
Ukiangalia kwa program endeshaji katika simu tuu, ni wazi kuwa Android na iOS zinafikia mpaka asilimia 99.1 ya mauzo ya simu janja zote.
Programu endeshaji ya Android ambayo inamilikiwa na mtandao wa Google bado ipo kileleni kwani inashikilia asilimia 86.2 ya mauzo ya simu janja

Mauzo ya simu zinazoendeshwa na program endeshaji za Windows na Blackberry yamezidi kushuka.
Niandikie hapo chini sehemu ya comment, je unahisi Android watazidi kuwa nambari moja katika kuongoza mauzo. Ningependa kusikia kutoka kwako