Picha za kunakili ukurasa ni njia mojawapo ya kupata kile ambacho kinaonekana juu ya uso wa kitu. Na wote wenye rununu zinazotumia iOS halikadhalika Android wamekuwa wakitumia njia huu kuweza kupata kile ambacho wanakihitaji kukitunza/kumtumia mtu mwingine kwa muda husika ama baadae.
Watumiaji mbalimbali wa Android 11 wenye simu janja za Samsung, Oppo, Xiaomi wamekuwa wakilalamika kuhusu picha za kunakili ukurasa kwenda moja kwa moja kuhifadhiwa Google Photos na hivyo kuongeza nafasi lakini pia kujaza nafasi kwenye memori ya simu.
Malamiko hayo ya watu wahusika wameyasikia na inaelezwa kuwa toleo la Android 12 halitaruhusu aina hiyo ya picha kuhifadhiwa kwenye memori iliyojulikana inapopatikana hasa.
Kwenye simu za Android kama mtu si mpekuzi wa kutaka kuweka vitu sawa basi picha zote ambazo zinaenda kwenye sanduku la Google la kutunzia picha linachukua kila kitu ambacho kinakuwepo ndani ya mfuko-DCIM.
Kwa kuwenda kwenye Google Photos>>Backup & Sync>>Backup folders mtu anaweza akachagua nini cha kupandisha kwa ajili ya kumbukumbu za baadae na kipi kiachwe nje.
Picha za kunakili ukurasa ni tafsiri yangu na isiyo rasmi nikimaanisha kile kitendo cha kutaka kupata nakala ya kile ambacho kinaonekana juu ya uso wa simu janja.
Waundaji wa Android 12 wanataka kumpa mtu uhuru zaidi wa kipi kinastahili kuingia kwenye Google Photos ambayo kwa mujibu wa takwimu ina picha zaidi ya trilioni 4 hadi sasa.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|
No Comment! Be the first one.