fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Alibaba Intaneti Teknolojia

Alibaba ni nini?

Alibaba ni nini?
Spread the love

Wengi tumewahi kusikia neno Alibaba lakini wachache wanaofahamu kuwa Alibaba ni nini. Alibaba ni soko la kibiashara mtandaoni  ambalo wauzaji na wanunuaji kutoka sehemu mbalimbali duniani hukutana na kufanya biashara.

Kampuni hii ya  Alibaba ilianzishwa mwaka 1999 na mmiliki wake Jack Ma. Kipindi inaanzishwa kampuni hii ilikuwa inatoa huduma moja tu kupitia tovuti yake ya Alibaba.com. Tovuti hii ilisaidia kuunganisha wauzaji wa bidhaa za kwenda nchi za nje waliopo nchini China pamoja na nchi nyingine na makampuni katika nchi zaidi ya 190.

SOMA PIA  Gmail kuja na barua pepe zinazofutika baada ya muda

Wasambazaji wa bidhaa hutumia tovuti ya alibaba kuuza malighafi au bidhaa zao za viwandani. Pia wanunuaji ni wale watu wanaonunua bidhaa rejareja au wauzaji bidhaa za jumla. Kuna sababu nyingi zinazoweza kupelekea mtu kununulia bidhaa zake alibaba ikiwemo unafuu wa bei, urahisi wa kutumia pamoja na wingi wa bidhaa za kuchagua.

Alibaba ni nini

Moja kati ya Ofisi za Alibaba nchini China

Tangu kuanzishwa kwake kampuni hii imekuwa ikikua na hii imepelekea kuongeza huduma zingine kama Alipay, Alimama, Taobao, Tmall, Freshipo, AliExpres, Lazada, Ding talk na zingine nyingi.

SOMA PIA  Pepsi wana mpango wa kuja na matangazo ya angani!

Endelea kutembelea tovuti yetu kufahamu zaidi kuhusu teknolojia pamoja na matumizi yake. Soma makala zetu nyingine hapa.

Semu Msongole

Digital Marketing Strategist, Content Writer, and Social Media Manager at Teknokona Blog.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania