Alama za vidole kimeo katika simu za Pixel 2 baada ya kusasisha Android 8.1

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Watumiaji wa simu za Pixel 2 XL ambao wamesasisha zimu zao kwenda Android Oreo wameripoti simu zao zinachelewa kufunguka pindi wanapotumia alama za vidole kufungua simu hizo.

 Pixel

Watumiaji Pixel 2 wanadai kwamba kabla ya kusasisha simu zao zilikua zinafunguka kwa uraisi kwa kutumia vidole lakini baada ya update hiyo imekuwa inachukua muda mrefu zaidi.

Tatizo hili limeripotiwa kwa wingi na watumiaji katika mabaraza mengi ya misaada katika mtandao, hali iliyopelekea baadhi ya wachangiaji kutoka Google kusema kwamba wanalifuatilia suala hilo.

INAYOHUSIANA  iPhone za mwaka 2019 zitakuaje? #Fununu

Swala hili ni pigo jingine kwa Google ambao ndio watengenezaji wa simu hizi, tayari simu za Pixel 2 zilisharipotiwa kuwa namatatizo ya kioo pamoja na spika miezi kadhaa nyuma. Hivyo hii pia inazidi kuharibu sifa ya Google hasa katika upande wa utengenezaji wa vifaa.

Tayari Google wamesema wanachunguza juu ya tatizo hilo na watatoa suluhisho karibuni, hivyo kama wewe ni mmiliki wa aina hiyo ya simu uwe macho katika ukurasa huu ili uweze kupata taarifa namna ya kutatua tatizo hili.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Comments are closed.