fbpx

AirPlay kuwekwa kwenye VLC Player

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Teknolojia inakuwa na lengo kuu likiwa ni kurahisisha mambo ili yaweze kwenda vizuri, programu kama VLC Player na AirPlay sio vitu vigeni kwa watu wanafuatilia teknolojia.

AirPlay ni nini?

AirPlay ni mkusaniko wa programu ambao unaruhusu mawasiliano kwa kutumia teknolojia isiyotumia waya kuona, kusikiliza au kutuma vitu kutoka kifaa kimoja hadi kingine.

VLC player

Vitu ambavyo AirPlay ina uwezo wa kuwasiliano navyo.

Sasa watumiaji wa vifaa vya Apple/Android watafurahi kutokana na kie ambacho kinaonekana kuwa kitawavutia wengi hasa kwa sababu VLC player imeshashushwa mara bilioni 3. Hii ni kwa sababu VLC watarajiwa kutoa sasisho ambalo litaruhusu mawasiliano kuka kwenye kifaa cha Apple/Android kwenda kwenye Apple TV.

Kwa lugha rahisi ni kwamba mtu mwenye bidhaa ya Apple/Android ataweza kutuma miziki, picha jongefu kutoka kwenye vifaa vyao kwenda kwenye Apple TV.

VLC player

Ushirikiano wa AirPlay pamoja na vifaa vingine.

Kujuisha kwa programu ya AirPlay kunatazamiwa kuja hivi karibuni kwani hakuna tarehe rasmi iliyotangazwa kuwa sasisho hilo litatoka. Je, wewe umepemdezwa na kitu hicho kipya kitakachokuja katika siku za usoni?

Vyanzo: The Verge, 9to5Google

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.