Kama wewe ni mtumiaji wa App ya Google Photos basi fahamu uwezo wa kuhariri picha zako utadhidi kuwa bora zaidi baadhi ya Google kuamua huduma ambazo zilikuwa kwa watumiaji wa Google Pixels tuu au wale wanaolipia huduma ya Google One, zinaenda kufunguliwa kwa watumiaji wote bure.
Hii inamaanisha kuwa unaweza kufurahia matumizi ya zana kama vile Magic Editor, Magic Eraser, na Photo Unblur bila malipo yoyote. Hii itakuwa kwa watumiaji wa Android na iOS.
Zana za AI za Google Photos kwa Wote
Awali, zana hizi za AI zilikuwa zinapatikana kwa simu za Pixel pekee na baadaye zilihitaji usajili wa Google One. Google One ni mjumuisho wa huduma ya kulipia inayousisha huduma ya Google Drive na Google Photos.
Google Photos ni huduma ya kuhifadhi picha mtandaoni inayowawezesha watumiaji wa Android na iOS kuwa na hifadhi (backup) ya picha na video zao.
Zana Maarufu za AI za Google Photos
- Magic Eraser: Hii hukuruhusu kufuta vitu au watu usiowahitaji kwenye picha zako. Usimwone tena yule mtu aliyejitokeza ghafla kwenye picha yako ya mwisho – mfute kwa kumgusa tu kwenye picha hiyo.
- Magic Editor: Zana hii hukuruhusu kuhariri picha zako kwa kutumia AI. Kupitia Magic Editor mtumiaji anaweza hamisha kitu kutoka eneo moja kwenda jingine katika picha.
- Photo Unblur: Zana hii hutumia AI kuboresha picha zilizopoteza umakini kwa kuchuja na kuimarisha picha. Unaweza kuitumia kwenye picha yoyote iliyo na ukungu na itaboreshwa kwa kuondolewa ukungu huo.
Pakua App ya Google Photos – Google PlayStore | Apple AppStore
No Comment! Be the first one.