fbpx
Afrika, Intaneti

5G Afrika Kusini: Huawei yapeleka teknolojia ya 5G Afrika Kusini

Sambaza

5G yaanza kupatikana katika nchi ya kwanza Afrika. Baada ya ‘figisu figisu’ za mataifa ya Marekani na baadhi ya washirika wake wa ‘kuibania’ kampuni ya Huawei juu ya usambazaji wa teknolojia yake ya kisasa zaidi ya mtandao wa 5G, kampuni hiyo imepeleka teknoljia hiyo nchi ya Afrika Kusini.

5G Afrika Kusini
Inaonekana kwa Afrika kampuni hiyo haitapata vikwazo au ugumu katika biashara ukilinganisha na katika mataifa ya magharibi

Huawei kwa kushirikiana na kampuni inayotoa huduma za mawasiliano ya nchini Afrika Kusini ya RAIN, wamefanikiwa kuwezesha teknolojia ya mtandao wa 5G nchini humo.

INAYOHUSIANA  Adhabu kutokana na aina ya kosa la mtandao

Hatua hiyo inaifanya nchi ya Afrika Kusini kuwa nchi ya kwanza ya Bara la Afrika kuwa na teknolojia ya mtandao wa 5G ambao una kasi zaidi ya mara 10 ya mtandao wa 4G.

Awamu ya kwanza ya usambazaji wa teknolojia hiyo itahusisha miji miwili kabla ya kusambazwa nchi nzima.

Maeneo muhimu ya miji ya Johannesburg na Pretoria ndio itanufaika na awamu ya kwanza ya usambazaji wa 5G.

INAYOHUSIANA  Kenya nayo yafikiria kudhibiti WhatsApp na Skype

Mtandao huo wa 5G unatarajiwa kuwa na kasi ya MB 200 kwa sekunde mpaka MB 700 kwa sekunde.

Mkurugenzi Mtendaji wa RAIN, amesema amefurahishwa na hatua ya uzinduzi wa teknolojia ya 5G nchini humo hususani kampuni yake ikiweka rekodi ya kuwa mtandao wa kwanza wa kuanzisha huduma hiyo.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.