fbpx

Uraibu kwenye Facebook: Namna ya kuzuia kuona machapisho Facebook

1

Sambaza

Katika vitu ambavyo ni vya kwanza unapoingia kwenye akaunti yako ya Facebook ni machapisho kutoka kwa marafiki, kurasa mbalimbali au hata matangazo lakini je, unafahamu ya kuwa unaweza kabisa ukazuia kuona machapisho kwenye Facebook?

Si kitu ambacho hakifahamiki kuwa machapisho mbalimbali yanavutia uso wa mbele kwenye mtandao wa kijamii maarufu sana duniani na wenye watumiaji wengi zaidi kila leo, Facebook. Inawezekana kabisa ukawa na uraibu wa kuona kuona machapisho na kukufanya kutumia muda mwingi sana ukiperuzi kuangalia walichochapisha marafiki zako kwenye ukurasa wa mbele wa Facebook (News Feed). 

Uraibu wa kwenye Facebook: Unaweza ukazuia kabisa kuona machapisho kwenye akaunti yako ya Facebook.

Kama ulikuwa unafikria namna gani unaweza kuzuia machapisho kwenye Facebook fahamu kuna programu ndogo iitwayo News Feed Eradicator. Hii ni programu ndogo ambayo inapakuwa na kuwepo kwenye kivinjari cha Chrome/Safari kama programu iliyoongezwa kwenye kivinjari (extension).

Ukitumia News Feed Eradicator bado utakuwa na uwezo wa kuona taarifa fupi (notification), maombi ya urafiki, ujumbe/jumbe kutoka kwa watu kwenye Facebook.

Kuzuia uraibu wa kuona machapisho Facebook: News Feed Eradicator itaondoa kabisa machapisho kutoka kwa marafiki zako.

Sasa  hii itakuwa ni mbinu na njia bora ya kuzuia uraibu wa kuona machapisho Facebook. Je, unafikiri programu hii itasaidia kwa kiasi gani kuondokana na ile tabia ya kutumia muda mrefu (uraibu) kuperuzi kwenye Facebook?

Chrome:|News Feed Eraicator, Safari|News Feed Eradicator

Vyanzo: Lifehacker, Post Planner

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Serikali ya Uingereza yatishia kufungia mitandao ya kijamii
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|