fbpx

Tetesi: Muonekano wa simu mpya za iPhone

0

Sambaza

Simu mpya za iPhone bado hazijatoka ni mpaka baadae mwaka huu lakini tayari kuna picha zilizovuja zikidaiwa kwamba ndio iPhone mpya zitakazozinduliwa miezi michache ijayo.

Ni wazi kwamba Apple ingependa kutofautisha kidogo muonekano wa iPhone (hasa kwenye uwekaji wa kamera zake) zijazo na zile ambazo tayari zimeshatoka. Kuna tofauti ya uwekaji wa kamera kwa simu moja na nyingine. Vioo vya simu zote vinaelezwa vitakuwa na teknolojia ya OLED.

Simu zinazodaiwa kuwa na mabadiliko ni iPhone X Plus na iPhone SE ambapo zinaelezwa kuwa na urefu wa inchi 6.1 na 6.5 kwenye kioo.

Kingine kinachoelezwa kwa simu hizo mpya za iPhone ni kwamba zitakuja na laini mbili kulingana mahitaji ya wateja wake wengi. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa simu za iPhone kuwa na laini mbili; zimezoeleka ni simu zenye laini moja tu.

Muonekano wa simu

Muonekano unaosadikiwa kuwa ni wa toleo lijalp la iPhone.

Ili kupata tarifa zaidi kuhusiana na ujio wa simu mpya za iPhone endelea kufuatilia teknokona na hususani wa uzinduzi wa simu hizo mwezi Septemba mwaka huu.

Tanzama picha jongefu hapo chini uweze kuona muonekano wa simu  toleo lijalo la iPhone litakuaje.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Motorola RAZR ipo njiani kuja lakini kivingine
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.