Marufuku ya matumizi ya mitandao ya kijamii

0

Sambaza

Serikali imewapiga marufuku watumishi wa umma kutumia mitandao ya kijamii wakati wa kazi kwa madai kuwa yanaathiri kasi ya mtandao wa intaneti ya serikali.

Mitandao ya kijamii haitapatikana kwenye intaneti ya serikali wakati wa muda wa kazi kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 9:00 alasiri.

Taarifa imeeleza chanzo cha kupiga marufuku ni kuwa kasi ya intaneti mtandao wa serikali inapungua kutokana na matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii hususani inayopakua video mfano YouTube na hivyo kusababisha watumishi wengine wanaotumia intaneti wa serikali wakati wa kutekeleza majukumu yao kupata changamoto.

Kwa taasisi zenye mahitaji maalum kwenye matumizi ya mitandao ya kijamii wakati wa kazi ziwasilishe maombi kwa Katibu Mkuu (Utumishi) wakiainisha watumishi wanaohitaji huduma hiyo na sababu za mahitaji hayo.

marufuku

Taarifa kuhusu matumizi ya mitadao ya kijamii wakati wa saa za kazi kwa taasisi za serikali.

marufuku

Taarifa kuhusu matumizi ya mitadao ya kijamii wakati wa saa za kazi kwa taasisi za serikali.

Hiyo ndio serikali, watanzania yufanye kazi kujenga taifa imara na bora. Je, hatua hiyo itasaidia kuongeza ufanisi katika kazi?

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Ijue sheria ya makosa ya mtandao mwaka 2015
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.