fbpx

Mambo yanayokera katika makundi ya WhatsApp

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

Sambaza

Palipo na watu wengi ni dhahiri kuwa vitu vingi vinaweza kutokea kutokea kutokana na kwamba kila mtu ana hulka yake kitu ambacho kinaweza kuleta mambo yanayokera.

Katika Dunia ya leo iliyojaa utandawazi WhatsApp imekuwa ni moja ya kiungi muhimu katika mawasilaiano ya haraka na mepesi kubwa zaidi kwa gharama nafuu sana lakini kwa wengine programu hiyo no kero kwao. Swali ni kwanini/kivipi?

>Mkuu wa Kundi
Mkuu wa kundi ndio ana mamlaka yote hivyo yeye ni muhimu kuweka kanuni zote zitakazoliongoza kundi.

Haitakiwi kuwepo kwa majadiliano baina ya mtu na mtu kwa sababu makundi haya yanajumuisha mawasiliano ya kikundi na sio ya mtu mmojam moja hivyo watu wawili wakiongea masuala yao peke yao kwenye kundi maongezi hayo yanaweza kuwakera wengine.

Suala la pili ni kwamba suluhisho ni rahisi ili kuepukana na usumbufu ambao unaweza kuwasababishia watu wengine kwa kumuandikia ujumbe binafsi mtu uliyemlenga na sio kwenye kundi.

Mambo yanayokera

Kwenye kundi la WhatsApp wana kikundi wanatakiwa kuweka ujumbe ambao unaweza kuwavutia/kumfurahisha kila mjumbe wa kundi hilo.

>Hakikisha kwamba unatuma ujumbe sahihi katika kundi sahihi.

INAYOHUSIANA  iPhone zinazokuja kuweza kuchaji bidhaa nyingine za Apple

Unaweza kuhakikisha mara ya kwanza na ya pili na hata mara ya tatu kabla hujabonyeza kitufe cha kutuma ujumbe. Kwa sababu usipokuwa makini unaweza kujiaibisha na hata kusababisha kujitoa kwenye kundi na kuwakwepa watu kwa muda ukifikiria aibu uliyoituma katika kundi la WhatsaApp.

>Usiwe mjumbe ambaye huchangii mijadala inayoibuka katika kundi.
Kwenye WhatsApp hakuna nafasi ya watu ambao hawashiriki katika kuchangia maelezo yoyote pale wanapopokea ujumbe na kuusoma bila kujibu. Hii inaleta ugumu pale ambapo wajumbe wengine kwenye kundi wanasubiri majibu kutoka kwa kila mmoja lakini mwisho wa siku wanaamua kukaa kimya.

>Muombe idhini mtu kabla ya kumkaribisha katika kundi
Hivi inawezekana kweli kuwakaribisha watu thelathini katika nyumba yako bila kuwafahamu? Kiuhalisia jambo hilo haliwezekani, vivyo hivyo na kwenye makundi ya WhatsApp ni lazima watu kuulizwa kama atapenda kujumuika kuwa miongoni mwa wana kikundi.

Mambo yanayokera

Na vile vile pale unapoondoka katika kundi ni vyema kusema sababu iliyosababisha ufanye uamuzi huo.

Je, ni jambo gani ambalo huwa linakukwaza katika makundi ya WhatsApp na namna gani unaweza kuepukana na kero hizo? Tuambie.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.