fbpx

Bei ya Samsung Galaxy Note 9 yavuja!

0

Sambaza

Kwa mujibu wa tovuti moja ya nchini Poland imeripoti kupata bei ya simu ya Samsung Galaxy Note 9 kutoka kwa mmoja wa mwajiriwa wa kampuni hiyo aliyehudhuria kikao cha ndani kuhusu maandalizi ya uzinduzi wa simu hiyo.

Kwa mujibu wa mfanyakazi huyo bei ya Samsung Galaxy Note 9 yenye ukubwa wa uhifadhi wa ndani  wa ukubwa wa 128GB na RAM GB 6 itakuwa ni $1,158 takribani shilingi za Tanzania 2,640,000.

Galaxy Note 9

Muonekano wa S-Pen ya Samsung Note 9

Samsung Note 9 inatarajiwa kuzinduliwa rasmi Agosti 9 mwaka huu ikiwa na prosesa mbili tofauti za aina ya Exynos 9810 na Snapdragon 845 kulingana na soko na inaelezwa itakuja na rangi tano tofauti tofauti. Hata hivyo, bado haipo wazi ni rangi gani hasa itakazokuja nazo.

INAYOHUSIANA  Huawei yaizidi Apple kimauzo

Kuvuja kwa bei ya Samsung Note 9 kutawasaidia wale wanaojiandaa kununua toleo hilo kwa kuweka vizuri akiba za mifuko yao.

Taarifa kamili na sahihi kuhusu wasifu wa Samsung Note 9 endelea kufuatilia hapa hapa teknokona tutakujuza karibuni.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.